Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO YASHIRIKI MAONESHO YA CHAMA CHA WATAFITI NA WAWEKEZAJI SEKTA YA MADINI CANADA


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse amezinadi fursa za uwekezaji katika sekta ya madini zilizopo nchini katika Maonesho ya Chama Cha Watafiti na Wawekezaji Sekta ya Madini Canada (PDAC) 2024 yaliyofanyika tarehe 3 hadi 6 Machi, 2024 jijini Toronto Canada.

Dkt Mwasse amebainisha fursa hizo wakati akitoa mada kupitia MineAfrica Inc kuhusu fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini nchini kwa wadau wenye nia ya kuifahamu Sekta ya Madini Tanzania.

Alifafanua kuwa fursa zilizopo kwenye Sekta ya Madini nchini ni utafutaji na uchimbaji wa madini muhimu na mkakati wa uanzishaji wa viwanda vya kuongezaji thamani na biashara ya madini. Ilieleza kuwa fursa hizo zinapatikana kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushirikiana na STAMICO.

Dkt. Mwasse ametumia fursa ya maoneshio hayo kukaribisha wawekezaji kushirikiana na STAMICO kwa kufanya ubia katika baadhi ya leseni za madini mkakati ambazo Shirika inamiliki kama lithium, iron ore, nickel, cobalt, graphtie, REE na copper.

Amewahakikishia wawekezaji watakaoshirikiana na STAMICO kunufaika na uzoefu wa Shirika wa zaidi ya miaka 50 kwa rig za kisasa inazomiliki na shirika ukaribu na wananchi na uelewa wa ufuatiliaji vibali nchini.

Pamoja na walisho hilo Dkt. Mwasse alitumia fursa hiyo kukutana na Bw. Thomas Ulm Mkurugenzi wa Multipower Products ya Canada inayojihusisha na kutengeza mitambo wa kuchoronga miamba.

Mazungumzo hayo yalilenga kujadili hatua za usafirishaji wa mtambo wa uchorongaji ulioagizwa na STAMICO ambapo Bw. Thomas Ulm alieleza kuwa Mtambo huo umekamilika na umeshasafirishwa mwishoni mwa Februari 2024.

Maonesho haya yalishirikisha wataalamu mbalimbali kutoka Tanzania akiwemo Kamishna Msaidizi Undelezaji Migodi Bw. Terence Ngole pamoja na wajumbe wengine kutoka Wizara ya madini na Taasisi zake.