News
STAMICO YATANGAZA FURSA KATIKA MAONESHO YA 58 YA KIMATAIFA YA BIASHARA ZAMBIA
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeshiriki maonesho ya 58 ya Kimataifa ya Biashara ya Zambia yanayofanyia mjini Ndola Maonesho hayo yenye dhima ya kufungua uwezo wa kiuchumu kupitia mashirikiano “unlocking economic potential through collaboration and partnership” yanafanyika viwanja vya maonesho ya Ndola kuanzia tarehe 26/06/2024 na yanatarajiwa kufungwa tarehe 2/7/2024. Mgeni Rasmi wa Maonesho hayo anatarajiwa kuwa ni Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema.
STAMICO imeshiriki kikamilifu kuonesha fursa zilizopo katika Shirika na nchi hasa mkaa mbadala wa Rafiki Briquettes na Makaa ya Mawe.