Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO YAWAFIKISHIA MKAA MBADALA WA RAFIKI BRIQUETTES WANA MWANZA


Shirika la Madini la Taifa ( STAMICO) limeshiriki Maonesho ya Wiki ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Rock City,Jijini Mwanza.
Kivutio kikubwa katika maonesho haya ni mkaa mbadala ambapo STAMICO iliwaelezea wananchi namna ya kutumia mkaa huu na mikakati iliyopo katika kuongeza uzalishaji. Pia STAMICO ilipika vyakula mbalimbali kutumia mkaa huu (live cooking).Wadau wengi wa madini kutoka mikoa mbalimbali pamoja na wakazi wa mwanza walinunua mkaa kwa wingi na pia wengine walionesha nia ya uwakala katika mikoa yao.Maonesho haya ya Wiki ya Madini yaliyoanza tarehe 3 Mei 2023 yanatarajiwa kufungwa rasmi tarehe 10 Mei 2023.