Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

TUZO YA MALKIA WA MADINI IMEZINDULIWA KWA KISHINDO MKOANI GEITA


*Wanawake kupewa kipaumbele asisitiza Waziri Mavunde*

Geita

Serikali imezindua rasmi tunzo ya Malkia wa Madini ya Chama cha Wanawake Wachimbaji wa Madini nchini (TAWOMA) iliyolenga kutambua mchango wa wanawake katika Sekta ya Madini.

Tuzo hizo zimezinduliwa rasmi Septemba 30, 2023 Mkoani Geita na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde zilizokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa TAWOMA

Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo Mhe. Mavunde ameipongeza TAWOMA kwa kuanzisha Tuzo hizi ambazo zitaleta hamasa kwa wanawake kushiriki kikamilifu katika mnyororo wa thamani wa madini.

Aidha, ameipongeza STAMICO kwa kuendelea kuwa walezi wazuri wa chama hiki na kuwawezesha kufanikisha kuanzishwa kwa tuzo hizi.

Alisema, Serikali kupitia STAMICO imewawezesha wanawake hao kushiriki kikamilifu na kuifanya TAWOMA kuonesha ukomavu ikilinganishwa na miaka ya nyuma ambapo TAWOMA ilikuwa ikisuasua.

Aliongeza kuwa, ifikapo mwaka 2030 kutakuwa na mabilionea wengi wanawake wachimbaji madini nchi nzima kwa kuwa tuzo hizi zinaenda kutia hamasa miongoni mwenu kushiriki kikamilifu kwa kufuata sheria na sera za uchimbaji salama wa madini.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Martin Shigella amefurahishwa na jitihada zinazofanyika ndani ya TAWOMA katika kuhakikisha wanawake wengi wanageukia fursa Ilizopo katika Sekta ya Madini.

''Mmemjengea heshima mwanamke mchimbaji na kupitia umoja huu mtazalisha mabilionea wengi na nitaendelea kutoa ushirikiano katika programu hii ya Malkia Wa Madini.

Kwa upande wa STAMICO, ambaye ni mlezi na msimamizi wa wachimbaji wadogo ameipongeza TAWOMA kwa kuwa wabunifu na kuja na Tuzo kama hizi ambazo zinakwenda kuleta matokeo chanya.

Vile vile, TAWOMA ni matajiri wa kesho kwa kuwa kila siku wanaangalia namna ya kuboresha chama ili kiwe na tija kwa wanachama wake nchini.

Kwa upande wa Chama cha Wanawake Wachimbaji Tanzania (TAWOMA) Mwenyekiti wa Chama hicho Bi. Semeni Malale amesema Tuzo hizi ni matokeo ya harakati za TAWOMA kuhamasisha uchimbaji bora na salama sambamba nakuongea ushiriki wa wanawake katika sekta ya madini.

Katika hatua nyingine, STAMICO ilipata tuzo ya kuwa mlezi bora kwa wachimbaji wadogo wakiwemo TAWOMA.

Mwishoni mwa mwezi Septemba 2023 TAWOMA chini ya usimamizi wa STAMICO imezindua tuzo ya Malkia wa Madini iliyoangazia maeneo ya Uchenjuaji Bora wa Madini migodini na mshindi ni Farida Mfuruki. Maeneo ya ulipaji Bora wa tozo na kodi mgodini imeenda kwa Mshikamano group yenye maskani yake.

Katika hafla hiyo fupi, tuzo zilizotolewa ni kipengele cha mtoaji huduma bora katika jamii zinazozunguka migodi ( CSR) mshindi alikuwa Alisi Salvatory na uzingatiaji Bora wa Afya na Usalama mgodini mshindi alikuwa Stella Herieth.