Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

UBUNIFU MAKINI WAIPA STAMICO USHINDI WA JUMLA



Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeibuka kidedea kwa kuwa mshindi wa jumla kwenye kipengele cha ubunifu makini (Overall Winner - Booth Creativity) katika maonesho ya 46 ya Sabasaba yaliyofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai 2022.

Tuzo hiyo ya STAMICO imetolewa tarehe 13 Julai 2022 na Mgeni rasmi Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kufunga maonyesho hayo.

Akipokea tuzo hiyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse alisema, tunajivunia kupata tuzo hii ya jumla kutokana na ubunifu makini wa bidhaa bora ya mkaa mbadala wa kupikia (Rafiki Briquettes) unaotokana na Makaa ya Mawe. Mkaa huu ni njia madhubuti ya kuepusha ukataji wa miti hovyo kwa ajili ya nishati.

Mkaa wa Rafiki Briquettes unaozalishwa na STAMICO ni Rafiki kwa mazingira, Rafiki kwa matumizi na Rafiki kwa bei.

Pamoja na tuzo ya ubunifu, STAMICO vilevile walipewa cheti cha ubora wa mpangilio wa bidhaa (Certificate of high display standard).

Huu ni ushindi mara pili mfululizo kwa kipindi cha miaka miwili, mwaka jana 2021 kwenye maonesho ya 45 ya Sabasaba STAMICO iliibuka mshidi wa kwanza wa jumla.

Tukio hili limehudhuriwa na mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugezi ya STAMICO Meja Jenerali ( Mstaafu) Michael Isamuhyo, pamoja na viongozi na wafanyakazi wa Shirika la Madini la Taifa.