Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

WACHIMBAJI, WAFANYABIASHARA NA WADAU WA MADINI WATEMBELEA SOKO LA KIMATAIFA LA YIWU NCHINI CHINA


*TAARIFA:*

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini

*NDUGU MSAFIRI MBIBO* ambaye ni kiongozi wa Msafara *(HEAD OF DELEGATION)* akiambatana na

*RAIS WA FEMATA NDUGU JOHN W. BINA* pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa *STAMICO* *Dkt. Venance Mwasse* na Makamu Mwenyekiti wa *BODI YA STAMICO* *Mhe. Lucas Lumambo Selelii* pamoja na ujumbe wa wadau wa madini, Agosti 14, 2023 wametembelea Soko la Kimataifa la Yiwu nchini China kujionea bidhaa mbalimbali zinazozalishwa kwa kutumia madini ikiwa ni sehemu ya kujifunza.

Bidhaa hizo ni pamoja na Madini ya vito, vifaa vya umeme, ikiwemo mitambo na vifaa vya Migodini majenerata, Compressors, mitambo ya kufua umeme na hewa Migodini pamoja na bidhaa zinazozalishwa Kwa Madini mbalimbali.

Ziara ya wadau wa madini nchini China inajumuisha wafanyabiashara wa madini, wachimbaji wadogo na wa kati wa Madini na watoa huduma migodini .

Aidha, mbali na wadau hao, pia, Watendaji wa Wizara ya Madini na Taasisi zake ikiwemo STAMICO,

Pamoja na Wawakilishi kutoka Taasisi za fedha.