News
WAZIRI BIASHARA NA MAENDELEO YA VIWANDA WA ZANZIBAR AIPA KONGOLE STAMICO KWA KULETA MKAA MBADALA VISIWANI.
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Mhe. Omar Said Shaaban amelishukuru Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa kupeleka Nishati Mbadala ya Mkaa unaotokana na Makaa ya Mawe Rafiki Briquettes kisiwani Zanzibar.
Mhe. Waziri ameyasema hayo alipokutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse katika viwanja vya Maisara wakati wa Tamasha la Biashara linalofanyika visiwani Zanzibar.
Ameitaka STAMICO kuainisha mawakala ambao wataendelea kupeleka mkaa huu huko Zanzibar na kujiwekeza vizuri ili biashara hii iwe endelevu kwani mkaa huu utakuwa mkombozi wa mazingira.