Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

WAZIRI MKUU AIPA KONGOLE STAMICO, AVUTIWA NA MKAA MBADALA WA RAFIKI BRIQUETTES


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (MB) leo Mei 09,2023 ametembelea banda la Shirika la Madini la Taifa ( STAMICO) kwenye Maonesho ya Siku ya Kilele cha Wiki ya Madini pamoja na Kongamano la Wachimbaji wa Madini yanayoendelea katika viwanja vya Rock City Jijini Mwanza.

Akiwa kwenye Banda la STAMICO Mhe. Waziri Mkuu alipata maelezo ya Mkaa mbadala wa Rafiki briquettes kutoka Kwa Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Venance Mwasse ambapo alieleza mchakato mzima namna utafiti Shirika lilianza utafiti wa Mkaa huu na hatimaye uzalishaji wa mkaa huu ulivyoanza na hatua ulipo sasa.Alieleza namna ubora ulivyozingatiwa na kwamba Shirika limepata cheti cha ubora kutoka TBS.

Akiongezea alieleza kuwa Shirika limeshaingiza mitambo miwili yenye uwezo wa kuzalisha tani 20 kwa saa kwa kila mtambo, Ambapo Mitambo hiyo inatarajiwa kufungwa katika Mikoa ya Pwani na Songwe.

Baada ya Maelezo hayo Mhe. Waziri Mkuu alifurahi na Kuipa pongezi STAMICO kwa kuja na Mkaa huu mbadala unaoenda kutatua na kudhibiti uharibifu wa Mazingira kwa kupunguza Matumizi ya mkaa unaotokana na Mti. Na hivyo akaita STAMICO kuendelea kuzalisha Mkaa huu kwa Wingi na kufunga Mtambo wa kuzalisha Mkaa katika Mkoa wa Ruvuma yanapozalisha Makaa kwa Wingi na kuutangaza ili kuweza kuwafikia Taasisi mbalimbali kama shule na Majeshi.

Maonesho hayo ya Wiki ya Madini yamefungwa rasmi tarehe 9 Mei 2023 na Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa (MB).