Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Madini la Taifa

*UJUMBE KUTOKA ZAMBIA WAVUTIWA NA KIWANDA CHA MWANZA PRECIOUS METALS REFINERY*

Imewekwa: 17 December, 2025
*UJUMBE KUTOKA ZAMBIA WAVUTIWA NA KIWANDA CHA MWANZA PRECIOUS METALS REFINERY*

Leo tarehe 26 Novemba 2025 – Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kupitia mradi wake wa ubia, kiwanda cha Mwanza Precious Metals Refinery, kilichopo Jijini Mwanza limepokea timu ya Ujumbe kutoka Lusaka nchini Zambia, ukiongozwa na Balozi wa Zambia nchini Tanzania, Mhe. Matheus Jere akiambatana na wawakilishi kutoka Wizara ya Madini kwa lengo la kujifunza kuhusu namna STAMICO inavyoendesha shughuli zake pamoja na usimamizi wa miradi yake. 

 

Akizungumza katika wasilisho fupi, Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance B. Mwasse alieleza namna Shirika linavyojiendesha kupitia miradi yake ikiwemo mradi mkubwa wa kutoa huduma ya uchorongaji na manufaa yanayopatikana kwa Shirika kuwekeza kwa niaba ya umma. Katika ziara hiyo, Dkt. Venance Mwasse aliambatana na Bw. Deusdedith Magala DHRA-STAMICO na Katibu wa kiwanda cha MPMR.

 

Kwa upande wake, Mhe. Balozi Matheus Jere alionesha kufurahishwa na namna Shirika linavyofanya kazi na kutoa pongezi kwa STAMICO na kiwanda cha MPMR. 

Vilevile, Mhe. Balozi ametoa rai kuwepo na Makubaliano ya Ushirikiano (MOU) kati ya STAMICO na ZCCM (Zambia Consolidated Copper Mines Ltd) hususan katika maeneo ya kubadilishana uzoefu.

 

Utendaji bora wa STAMICO umeendelea kuwavuta mataifa mbalimbali kuja kujifunza namna Serikali inavyoweza kusimamia na kushiriki katika uvunaji wa rasilimali madini kwa manufaa ya taifa lake.

 

Mrejesho, Malalamiko au Wazo