Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

RAFIKI BRIQUETTES YA STAMICO KUANZA KUTUMIKA KATIKA MAGEREZA YA UGANDA


▪️Yapokelewa kwa Kishindo

▪️Kamishna Jenerali atoa maelekezo kwa maafisa wake kufanya taratibu za kuipata Nishati hii kwa haraka.

▪️Awahimiza kufanya ziara Tanzania kujifunza zaidi kuhusiana na Nishati hii

▪️MD awahakikishia uwezo wa STAMICO kuzalisha na kuhakikisha Nishati inapatikana kwa wingi.

Kampala, Uganda 25/9/2205

Mkuruzenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa ( STAMICO), Dr Venance Mwasse akiongozana na Bi Haika Shishira, Mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda, Mha Baraka Manyama, Kaimu Mkurugenzi wa Migodi na Shughuli za Kihandisi, Bw Alex Rutagwelela, Mkuu wa Uchorongaji na Bwn Deus Alex, Meneja Masoko na Mahusiano ya Umma, tarehe 25 Mwezi Septemba walifika katika ofisi ya Makao Makuu ya Magereza nchini Uganda. Katika ziara hiyo Dr Mwasse pamoja na ujumbe wake walipokelewa na Kamishna Jenerali wa Magereza Bwn Bwabushaija pamoja na maafisa wengine waandamizi.

Katika ziara hiyo , Dr Mwasse alimuelezea Kamishna Jenerali wa Magereza kuhusiana na Shirika, Ubunifu uliofanywa na STAMICO kuyatumia makinikia ya Makaa ya mawe na kutengeneza Nishati Safi ya Kupikia, mafanikio ambayo Nishati hii safi imeyapata mpaka sasa.

Dr Mwasse alimuelezea Kamishna Jenerali kuhusiana na Magereza zote 129 za Tanzania pamoja na taasisi nyingine kuwa wanatumia Nishati ya Rafiki Briquettes.

Dr Mwasse pamoja na wataalamu wake kutoka waliezea kwa undani jinsi Nishati hii inavyofanya kazi na kuwaka zaidi ya masaa ma nne.

Kamishna Jenerali alifurahishwa na ufanishi ambao alikuwa ameelezewa na kuwataka maafisa wake wapate Sampuli za Nishati hii na wapange safari kwenda Tanzania kujifunza zaidi na kujionea kwa macho kiwanda kilipo.

Kamishna Jenerali aliushukuru Ujumbe wa STAMICO kwa kuwatembelea lakini pia kwa kuwaonyesha njia mbadala itakayowawezesha kupunguza gharama zao za kununua Nishati za kupikia.

STAMICO inaendelea na nia yake madhubuti ya kuongeza masoko kwa bidhaa zake za Makaa ya mawe, Rafiki Briquettes na huduma za uchorongaji.