Historia
Historia
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) linamilikiwa na Serikali, lilianzishwa Mwaka 1972, kwa lengo la kusimamia maslahi ya Serikali katika Sekta ya Madini. Tarehe 5 Machi, 2015, Amri ya Kuanzisha Shirika (The Public Corporation State Mining Corporation Establishment Amendment Order, 2015) ilifanyiwa marekebisho na kulifanya Shirika kuwa chombo madhubuti cha kuwekeza katika Miradi ya Kimkakati ya Madini (Mining Strategic Projects) ili kuongeza mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa.