STAMICO, GGM NA CAPITAL DRILLING ZASHEHEREKEA MIAKA ZAIDI YA MIWILI BILA MAJANGA KATIKA KAZI
Shirika la Madini la Taifa ( STAMICO) limeungana na Geita Gold Mine ( GGM) na Capital Drilling kusherehekea kutimiza miaka zaidi ya miwili bila kupata majanga katika kazi( Free Loss Time Injury) katika mgodi wa GGM Mkoani Geita.
Hafla hiyo ya kupongezana kwa mafanikio haya, imefanyika leo tarehe 24/7/2026 katika eneo la STAMICO ndani ya Mgodi wa GGM mjini Geita na kuhudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi.
Akiongea katika hafla hiyo, Dkt. Mwasse alianza kwa kumshukuru Mungu kwa kufikia siku hii yenye mafanikio makubwa .
"Mwaka 2024, Mwezi wa tano tulipata majanga hapa na tulijiapiza kujitahidi kufanya kazi kwa usalama zaidi kujiepusha na majanga mbali mbali. Leo kusimama hapa ni juhudi kubwa ambazo zimefanywa kwa ushirikiano mzuri kati ya STAMICO, GGM na Capital Drilling" alisema Dkt Mwase.
Dkt Mwasse amewapongeza Watumishi wa STAMICO kwa juhudi kubwa wanazozifanya na kutambua mchango wao.
Amewaahidi kuwapa ushirikiano katika kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii na akawahasa kutobweteka na mafanikio haya.
Naye, Mkurugenzi wa Jiologia kutoka GGM Bi. Janet Luponela amewahimiza STAMICO kukazana kufikia utamaduni wa hali ya juu wa usalama ( Resilience Safe Culture) pia wazidishe nidhamu na kudumu katika mafanikio.
STAMICO inaendelea kuhakikisha katika miradi yake yote suala la Usalama linapewa.