Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Madini la Taifa

STAMICO YAPEWA CHETI CHA SHUKURANI KWENYE USIKU WA MADINI

Imewekwa: 12 March, 2025
STAMICO YAPEWA CHETI CHA SHUKURANI KWENYE USIKU WA MADINI

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) jana tarehe 20 Novemba limepokea cheti cha shukurani kwa Udhamini wa Usiku wa Madini. Cheti hicho kimetolewa na Wizara ya Madini kwa kushirikiana na Tanzania Chember of Mines.

Cheti hicho kimekabidhiwa na Waziri wa Madini na Uchumi wa Buluu wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Ali Hassan Joho. Usiku huo wa Madini ulifanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Madini wa Tanzania Mhe. Anthony Mavunde.

Aidha Cheti hicho cha Shukurani kwa Udhamini wa Usiku wa Madini kilipokelewa na Ndg. Deusdedith Magala, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala STAMICO, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, CPA Dkt. Venance Mwasse.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo