Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Madini la Taifa

STAMICO YASHIRIKI MKUTANO WA MADINI NA UWEKEZAJI

Imewekwa: 12 March, 2025
STAMICO YASHIRIKI MKUTANO WA MADINI NA UWEKEZAJI

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeshiriki kwenye Mkutano wa Madini na Uwekezaji kwa kuwaleta pamoja wadau wake kwenye eneo moja.
Mkutano huo wa siku tatu ulioanza tarehe 19 Novemba 2024 unafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
STAMICO imeonyesha huduma na biashara zake kama vile nishati safi ya kupikia ya Rafiki Briquettes, mitambo ya uchorongaji na huduma kwa wachimbaji wadogo.
Mkutano huo uliofunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa utamalizika tarehe 21 Novemba 2024.
Kwenye banda kubwa la STAMICO ambalo limepewa jina la Stamico Village, wachimbaji wadogo na vyama vya wajasiriamali walioko kwenye mnyororo wa thamani wa madini wameshiriki kwa udhamini wa STAMICO.
Wadau hao ni pamoja na Chama cha Wachimbaji Wanawake (TAWOMA), Women in Mining Operations (WIMO), na Dacorema.
Wengine ni Morogoro Region Miners Association (MOREMA) na Wachimbaji wadogo kutoka Mkoa wa Lindi.
Washiriki wamejipanga kwa kuonyesha bidhaa mbalimbali kwenye sekta ya madini.
STAMICO imebuni utaratubu wa kushiriki kwenye maonesho makubwa kwa kuwaleta pamoja wadau wake na hasa wachimbaji wadogo.
 

Mrejesho, Malalamiko au Wazo