News
STAMICO YAPATA TUZO MKUTANO MKUU WA WAJIOLOJIA TANZANIA
Shirika la Madini la Taifa(STAMICO) limepata tuzo ya Mchango Mkubwa katika ufadhili na kuwezesha Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wajiolojia Tanzania (TGS)
Tuzo hiyo imekabidhiwa leo tarehe 4 Disemba 2024 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO DKT. Venance B. Mwasse na Mgeni rasmi wa Mkutano huo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Bw. Msafiri L. Mbibo.
Wakati hakipokea Tuzo hiyo Dkt. Mwasse alielezea Umuhimu wa Wajiolojia katika Kukuza Sekta ya Madini nchini.
“_Hakuna uchimbaji wowote unaweza kuanza pasipo kuwa na taarifa za Kijiolojia ambazo zinatokana na kazi za Wajiolojia”_ Alisisitiza Dkt. Mwasse na Kuwaidi Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) litaendelea kuwa bega kwa bega kusaidia Jumuhiya ya Wajiolojia kwa Maslai mapana na kuendeleza Sekta ya Madini na Taifa kwa Ujumla.
Katika kuhitimisha Dkt. Mwasse alisema Shirika litaendelea kushiriki kwenye sekta ya Madini kwa ajili ya manufaa ya Taifa na Watanzania.