News
STAMICO YATIA FORA MAONESHO YA NANE YA MADINI MKOANI GEITA KWA TUZO DABO DABO
- *Yanyakua jumla ya Tuzo 8*
- *Mgeni Resmi aipongeza*
- *Wadau STAMICO & Kijiji Wamtunuku MD Keki ya Shukrani*
Shirika la Madini la Taifa ((STAMICO) pamoja na wadau wake wametwaa jumla ya tuzo Nane katika Maonesho ya Teknolojia ya Madini yakiyofikia tamati leo katika Viwanja vya Dkt.Samia Suluhu Hassan Mkoani Geita.
Tuzo hizo ni Mshindi wa Kwanza wa Jumla taasisi za Umma (Banda Bora), Mshindi wa Kipekee wa Jumla wa Uwezeshaji Makundi Maalumu ,Kampuni kubwa ya Uchimbaji madini na Ujenzi wa Miundombinu ya kudumu ya Maonesho ya Madini Geita.
Tuzo nyingine ni taasisi Wezeshi ya Serikali, Mteja wa thamani kutoka GF Trucks & Equipment.
Wadau ambao walishiriki kwenye maonesho haya chini ya mwavuli wa STAMICO na kupata tuzo ni TAWOMA na Tanzania Youth in Mining.
Tuzo hizi za kipekee zinatokana na utendaji dhabiti wa Shirika chini ya usimamizi wa Dkt.Venance Mwasse Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO katika kutekeleza Dira ya Wizara ya Madini ya Vision 2030 ambayo ni utekelezaji wa Maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Mwaka jana,STAMICO pamoja na wadau wake walioshiriki kwenye eneo moja ilizoa tuzo 6.
Shirika limekuwa kinara katika uendelezaji wa makundi maalumu ya wachimbaji wadogo Wanawake na Vijana, Walemavu wenye usikivu hafifuna watu wenye ulemavu wa ngozi.
Hafla ya utoaji tuzo imefanyika leo tarehe 28 Septemba,2025 katika Viwanja vya Maonesho ya Madini vya Dkt.Samia Suluhu Hassan mkoani Geita ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko.
Katika hotuba yake,
Dkt.Doto Biteko amewapongeza STAMICO kwa kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya Madini kupitia tasnia ya Uchorongaji.
Amesema kuwa STAMICO ni mfano wa kuigwa kwa namna wanavyosaidia nchi katika uingizaji wa teknolojia za kisasa katika sekta ya Madini. STAMICO wameweza kuondoa dhana potofu kwa watanzania hatuwezi kufanya baadhi ya kazi.
Shirika kwa sasa linatekeleza mkakati wake wa kujiendesha kibiashara na kushiriki kikamilifu katika uchorongaji na uendelezaji miradi yake ya uchimbaji madini.
Kauli mbiu ya maonesho ya mwaka huu ni " Ukuaji wa Sekta ya Madini ni Matokeo ya Matumizi ya Teknolojia sahihi na Uongozi Bora,Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025.