Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Madini la Taifa

KIKAO CHA WATUMISHI WA STAMICO

Tarehe 19/07/2024 Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) lilifanya Kikao cha Watumishi wote wa Shirika hilo ambacho kilifanyika katika Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma. Kikao hicho ambacho kilikuwa na tija kubwa kwa Shirika kwani kilijadili mipango mingi ya Shirika na namna gani ya kuweza kuweka mipango madhubuti ili kulifanya Shirika liweze kuwa imara na kuwa na mchango mkubwa kwa Serikali katika kuleta maendeleo ya nchi na kuchangia pato la Taifa kwa kiasi kikubwa kupitia Sekta ya Madini. Kikao hicho pia kilikuja na Azimio la Shirika kuanza kujitegemea lenyewe,ikiwemo kujilipa mishahara pasipo kutegemea kutoka Serikalini. Pia kikao kiliwataka Wafanyakazi wa Shirika kuwa wabunifu ili kuleta tija na kuongeza kipato cha Shirika ili kuisaidia Serikali katika maendeleo ya Taifa. Kikao hicho kilikuwa chini ya Mwenyekiti CPA DKT, Venance Bahati Mwasse ambaye pia ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
Mrejesho, Malalamiko au Wazo