Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

WAZIRI JAFO AIPAISHA AJENDA YA RAFIKI BRIQUETTES


*Aipongeza Wizara ya Madini kushiriki kwa vitendo jitihada za kupambana na uharibifu wa mazingira kupitia mkaa Mbadala wa Rafiki Briquettes

*Aipongeza STAMICO kupanda na kutunza miti katika Bustani za Dodoma na Geita.

Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Seleman Jafo amelipongeza Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuongeza mitambo mikubwa ya kuzalisha Mkaa mbadala na kutekeleza kwa vitendo maagizo aliyoyatoa kwenye uzinduzi wa Kampeni ya STAMICO na Mazingira At 50 wakati wa Maadhimisho wa Miaka 50 ya STAMICO.

Amesema STAMICO imesimamia vizuri miti yote iliyopandwa katika bustani zake na wameweka fensi ili kuzuia uharibifu wa miti hiyo jambo linalofanya miti hiyi kukua vizuri.

" Mimi nimeenda kutembelea bustani ya Dodoma kimya kimya bila kuwajulisha lakini mmefanya vizuri sana katika eneo lile" Mhe. Jafo

Ameongeza kuwa ajenda ya mkaa wa Rafiki Briquettes wa STAMICO umeifanya Wizara ya madini kusaidia sana katika kutunza mazingira hivyo hakuna budi ya kwenda na ujenda ya pamoja ya Madini na Mazingira.

Ameitaka STAMICO kurahisisha upatikanaji wa mkaa huo mbadala ili uweze kuwafikia watu wote kwa wakati wowote.

Mhe Waziri amelishukuru Shirika kwa kufanya kazi kwa pamoja na vikundi mbalimbali Kama vile Kikundi cha Wanawake na Samia ambao wameisimamia kutunza miti 560 katika eneo la EPZA.

Nitoe rai tena kwenu STAMICO kuja na mbinu nyingine ya kupeleka vitalu vya miti mashuleni ili miti iweze kupandwa na kuhudumiwa huko.

Kwa upande mwingine Mhe. Jafo ameitaka STAMICO kuendelea kutoa elimu ya matumizi ya chuma badala ya magogo katika kuimarisha miamba wakati shughuli za uchimbaji mdogo wa madini zikiendelea.

Katika tukio hilo la upandaji miti jumla ya miti 340 iliweza kupandwa na Mhe Jafo na Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde,pamoja na viongozi wengine wa chama na Serikali. Miti hiyo imepandwa katika Viwanja vya bomba mbili (EPZA).