STAMICO YATWAA TUZO KWA KUWA MDHAMINI MKUU WA JUKWAA LA TANO LA LOCAL CONTENT
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limepata tuzo na cheti kutokana na kuwa mdhamini mkuu wa jukwaa la Local Content lililowakutanisha wadau wa sekta ya madini nchini lililofanyika kuanzia tarehe 22 hadi 24/07/2026 jijini Mwanza.
STAMICO imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wananchi wanapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali katika sekta ya madini.
Tuzo hiyo iliyotolewa na waandaji wa jukwaa hilo Tume ya Madini imetolewa na Mgeni Rasmi Dkt. Abdulrahman Mwanga ambaye ni kamishna wa madini wakati akifunga jukwaa hilo lililofanyika kwa siku tatu jijini Mwanza imeonyesha ni jinsi gani STAMICO inavyoendelea kutekeleza majukumu yake kwa kutekeleza maagizo ya Serikali katika sekta ya madini ili kuchangia pato la Taifa na kuinua uchumi wa Watanzania.
STAMICO itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuliletea taifa maendeleo kupitia sekta ya madini.