Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

SEMINA YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI KUHUSU MAJUKUMU YA STAMICO NA GST, NA MoU ILIYOINGIWA KATI YA TAASISI HIZO


Kamati ya KUDUMU ya Bunge ya Nishati na Madini leo tarehe 10/02/2024 imepata Semina elekezi kuhusu Utofauti wa Majukumu ya STAMICO na GST pamoja na Hati ya makubaliano iliyopo kati ya Taasisi hizi mbili na utekelezaji wake. Katika Semina hiyo kumetolewa ufafananuzi wa kina juu ya majukumu ya kila Taasisi kimuundo. Aidha, STAMICO imeeleza kwa kina kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa miradi yake ya maendeleo.

Akiwasilisha andiko lake katika Semina hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO CPA, Dkt. Venance B. Mwasse, ameeleza miradi inayoendeshwa na STAMICO na matokeo makubwa ambayo STAMICO imeyapata. Pamoja na hatua zilizofikiwa, ameainisha pia changamoto za kitaasisi katika kutimiza majukumu ya kila siku.

Kwa upande wake, Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde ameipongeza STAMICO kwa kuendelea kutekeleza majukumu yake vizuri na pia amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada alizozifanya kufanikisha ununuzi wa mitambo na vifaa vya uchorongaji kwa ajili ya wachimbaji wadogo ambavyo vimekuwa msaada mkubwa.

Pia, ameiomba Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kutafuta wasaa ili Wizara ya Madini iwapitishe wajumbe katika sheria ya Madini ili kuondoa muingiliano wa kimaamuzi na Sheria ya Ardhi pale Mwananchi anapohusishwa kwenye "Mineral Rights na Land Rights" ili iwe rahisi kuwahudumia wananchi wanapokuwa katika majimbo yao.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Dkt. David Mathayo (Mb) amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO pamoja na timu yake kwa hatua kubwa waliyoipiga katika kuendeleza miradi ya Shirika na kuwataka kuimarisha ushirikiano mkubwa uliopo kati ya GST na STAMICO.