Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO NA KOMIR YA KOREA WAINGIA MAKUBALIANO KUENDELEZA MADINI YA KIMKAKATI NCHINIShirika la Madini la Taifa (STAMICO) leo Juni 4, 2024 limesaini hati ya makubaliano (MoU) na Shirika la Ukarabati wa Migodi na Rasilimali za Madini la nchini Korea (KOMIR) ili kuendeleza rasilimali madini ya kimkakati nchini pamoja na kubadilishana uzoefu.

Hati hiyo imesainiwa jijini Seoul nchini Korea kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse na Rais ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa KOMIR Bw Hwang, Kyu-Yearn na kusimamiwa na Waziri wa Biashara,Viwanda na Nishati wa Korea Kusini Bw.Inkyo Cheong.

Makubaliano hayo ni ya miaka mitatu na hati hiyo itahusisha ushirikiano kwenye uendelezaji wa madini ya kimkakati na kubadilishana uzoefu.

Makubaliano hayo ni matunda ya uhusiano wa muda mrefu kati ya nchi hizi mbili pamoja na ziara rasmi ya kikazi ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan nchi ya Jamhuri ya Korea iliyoanza rasmi tarehe 2 June 2024 na kutarajiwa kuhitimishwa tarehe 6 June 2024.

Katika hafla hiyo MD wa STAMICO Dkt Mwasse amesema Tanzania na Korea zimelenga kushirikiana katika masuala ya utafiti, uwekezaji, uchimbaji na kujenga uwezo wa kuongeza thamani ya madini ya kimkakati yanayopatikana nchini Tanzania.

Ikumbukwe STAMICO ni miongoni mwa Taasisi zilizoshiriki katika ziara rasmi ya kikazi ya Mhe Rais nchini Korea ya Kusini na kupitia utiaji sahihi wa hati hii utaongeza chachu katika masuala ya tafiti za Madini ya kimkakati kama vile *graphite,Lithium,Nikel/Cobalt,Manganese*,nk pamoja na uchimbaji, Uchenjuaji na biashara ya Madini kwa u jumla kati ya nchi hizi mbili.