News
STAMICO YAPONGEZWA NA CHAMA CHA WACHIMBAJI MADINI WANAWAKE (TAWOMA) MKOA WA TANGA
*Leo tarehe 15/08/2024* Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt.Venance Mwasse amefanya kikao kazi na Wachimbaji Wadogo Wanawake mkoa wa Tanga akiwa ameambatana na Kaimu Afisa Madini Mkazi mkoa wa Tanga Mhandisi Jackson R. Shirima.
Katika kikao hicho Dkt Mwasse alieleza dhamira ya Shirika ya kusaidia Wachimbaji Wadogo Wanawake kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli za uchimbaji madini.
Akitatatua changamoto ya ukosefu wa maeneo ya uchimbaji Dkt. Mwasse amewaelekeza Wachimbaji hawa kuomba leseni kupitia Tume ya Madini.
Kupitia STAMICO wachimbaji wanawake wa Mkoa wa Tanga watawezeshwa gharama za awali ili wapate maeneo ya uchimbaji hususani madini ya chokaa na ujenzi yanayopatika kwa wingi mkoani Tanga.
Katika kuonesha dhamira ya *Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani kuona wanawake wanashiriki kwenye shughuli za uzalishaji Dkt. Mwasse amekubali ombi la TAWOMA Mkoa wa Tanga kuwalipia deni lao la Leseni ya uchimbaji madini Chokaa wanalodaiwa.
*Sambamba na hilo Shirika liko tayari kuwanunulia Mashine za Posi tano(5) za kulipia mirabaha ya Serikali na kuwasaidia kupata Leseni mpya wanazozihitaji kwa kushirikia na Mamlaka za utoaji Leseni amesema hayo baada ya kupokea changamoto mbalimbali zinazowakabili wachimbaji hao mkoani Tanga kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Wanawake mkoa wa Tanga Bi. Mariam Mshana.
Akaendelea kusema mpango wa Shirika ni kuhakikisha Wachimbaji Madini Wanawake wananufaika na raslimali ya Madini huku akifafanua wanawake ni jeshi kubwa na Shirika linaamini ukiwasaidia wanawake umesaidia jamii kwa kiasi kikubwa Kutokana na idadi yao kuwa kubwa ukilinganisha na wanawaume kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya Mwaka 2022.
Hii pia ni jitahada za Shirika katika kuunga mkono maelekezo na juhudi mbalimbali za Wizara ya Madini kupitia Waziri wa Madini *Mhe. Antony Mavunde (Mb.)
*Kwa upande wake Mwenyekiti Chama cha wachimbaji Wanawake Mkoa wa Tanga (TAWOMA) Bi. Mariam Shirima amelipongeza Shirika la Madini la Taifa kwa kuendelea kusaidia wachimbaji Wadogo Wanawake na kusema wanajivunia kuwa na mlezi STAMICO ambapo mwaka 2023 tulipokea mtambo wa kuchakata mawe ya Dhahabu ambao kwasasa unafanya kazi Wilayani Kilindi na leo tumehakikishiwa kulipiwa madeni na kutafutiwa Leseni mpya.
*Mwishoni Bi. Mariam aligusia katika mkoa wa Tanga tunao akinana mama ambao wamepata mikopo kutoka katika taasisi za kifedha na kusema haya ni matunda ya jitihada za STAMICO katika kuwakomboa Wachimbaji Madini Wanawake.