Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO YASHIRIKI KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAZINGIRA


Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) linashiriki katika maadhimisho ya Wiki ya Mazingira kitaifa Jijini Dodoma yaliyoanza tarehe 1/6/2024.

Uzinduzi rasmi wa maadhimisho haya ulifanyika tarehe 3/6/2024 na mgeni rasmi akiwa ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko.

Katika uzinduzi wa mabanda ya maonesho, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametoa wito kwa idara na vitengo vya mazingira katika wizara na taasisi za serikali kuendelea kutekeleza majukumu yao ya msingi yanayolenga kuleta suluhisho la athari za Mazingira nchini.

Sambamba naye aliambatana na viongozi wengine wa kiserikali akiwemo Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira, Dkt. Seleman Jafo, na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule.

Kauli mbiu ya maonesho haya ni "Urejeshwaji wa ardhi iliyoharibiwa na ustamimilivu wa hali ya Jangwa na Ukame."

Kilele cha maadhimisho haya kitakuwa tarehe 5/6/2024 na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Raisi Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango.