News
TANZANIA YAN’GARA MIRADI YA KINYWE
Ripoti ya Benki ya Dunia Yaitaja ya Tatu Afrika, Sita Duniani
Tanzania yatoa Somo mwelekeo sahihi nchi za Afrika katika Uwekezaji, uvunaji wenye maslahi kwa Wananchi
Yasisitiza ushirikiano baina ya nchi za Afrika
Capetown
Ripoti ya Benki ya Dunia na Takwimu za Taasisi ya Jiolojia ya Marekani kuhusu makisio ya utajiri wa mashapo ya Madini ya Kinywe ifikapo mwaka 2050 imeitaja nchi ya Tanzania kushika nafasi ya Sita (6) Duniani na nafasi ya Tatu (3) Afrika huku Msumbiji ikishika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Madagasca kwa upande wa nchi za Afrika.
Hayo yamebainishwa Novemba 7, 2024 na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dkt. Venance wakati akimwakilisha Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde.