Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

WAZIRI WA MADINI MHE MAVUNDE AIPONGEZA BODI YA WAKURUGEZI YA STAMICO


Waziri ya Madini Mhe Anthony Mavunde Leo tarehe 30 Januari 2024 amekutana na Bodi ya Wakurugezi ya STAMICO china ya Mwenyekiti wake Mej Gen (Mstaafu) Michael Isamuhyo pamoja na Menejimenti na kuipongeza Bodi kwa kazi kubwa waliofanya kwa kulisimamia Shirika vizuri na kulifanya ligare kwenye ramani ya Tanzania.

Kazi kubwa mmefanya STAMICO ilikuwa inaondoka kwenye ramani na kuna wakati Shirika lilikuwa lifutwe kutoka na kutokuwa na tija kwa Serikali lakini sasa tunajivunia utendaji mzuri wenye tija. Naipongeza Bodi, Menejimeti na Wafanyakazi wa Stamico kwa kazi nzuri mnayofanya alisema Waziri Mavunde.

Alipongeza Shirika kwa kupanda kwa ufanisi mkubwa tukio la uzinduzi wa mitambo kwa Wachimbaji wadogo tukio ambalo Mgeni rasmi alikuwa Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan.

STAMICO limeweza kuongeza mapato yake kutoka Billion 1.4 hadi Billion 61 kwa Kipindi cha miaka minne iliyopita na kuweka kutoa gawio jumla ya Shilingi Biliion nane.

Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO Meja Gen (Mstaafu) Micheal Isamuhyo amemshukuru Mhe Waziri pamoja na uongozi mzima wa Wizara kwa jinsi wanavyo shirikiana vizuri na Shirika ikiwa pamoja na maagizo

mbalimbali mnayotupatika katika kuendeleza sekta ya Madini nchini

Kikao hiki kimefanyika Dodoma kwenye ukumbini wa Jakaya Kikwete wakati wa kikao cha kawaida cha 18 Kati ya Bodi na Menejimenti ya Stamico.