Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

BODI YA STAMICO YAVUTIWA NA UTENDAJI WA SHIRIKA


Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ikiongozwa na Mwenyekiti wake,Meja Jenerali (Mstaafu) Michael Isamuhyo leo Julai 31 wametembelea miradi mbalimbali ya Shirika ili kujionea utekelezaji.

Akizungumza katika msafara huo, Mwenyekiti wa Bodi amesema wameridhishwa na utendaji kazi wa Shirika katika kutekeleza miradi mbalimbali kwa ufanisi.

Bodi hiyo imetembelea viwanja vinavyomilikiwa na Shirika vilivyopo jijini Dar es Salaam pamoja na kiwanda cha kutengeneza mkaa mbadala wa kupikia wa Rafiki Briquettes uliopo Wilaya ya Kisarawe,Mkoa wa Pwani.

Shirika pia lipombioni kujenga viwanda vya aina hiyo katika mikoa ya Dodoma,Tabora na Songwe.

Ameongeza kuwa mafanikio haya ni kielelezo kuwa bodi na menejimenti wanafanya kazi kwa pamoja.

“Niwapongeze sana menejimenti kwa niaba ya bodi kwa mafanikio haya makubwa”, alisema.

Pia ameshauri menejimenti kuandaa kumbukumbu za waasisi wa Shirika na kuandika kitabu kitakachoeleza ....