Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YAIPONGEZA STAMICO KWA KIWANDA CHA MKAA MBADALA.


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wametembelea na kukagua kiwanda cha kuzalisha mkaa mbadala wa makaa ya mawe (Rafiki Briquettes)

kilichopo Msasani, jijini Dar es salaam.

Kamati hiyo ilitembelea kiwanda hicho siku tarehe 14 Machi 2022 na kupokelewa na viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Madini na Shirika la Madini la Taifa wakiongozwa na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa, Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo.

Akiongea mara baada ya kutembelea kiwanda na kujionea jinsi kiwanda hicho kinavyofanya kazi Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Dustan Kitandula ameipongeza STAMICO kwa kuwa na ubunifu ambao unalenga kuchangia katika jitihada za kutunza mazingira, kuongeza ajira na kuongeza nishati ya kupikia.

Amesema ubunifu wa STAMICO ni mkubwa na unahitaji pongezi kwa kuwa unakuja kuchangia katika ongezeko la nishati kidigitali nchini.

Amesema STAMICO inatakiwa kuongeza kasi na kukamilisha taratibu za uzalishaji ili iweze kuipeleka bidhaa hii sokoni kwa kuwa ina uhutaji mkubwa sana sokoni

Aidha ameitaka STAMICO kutanua wigo wa soko kwa kufanya kampeni ya kutosha ili watumiaji waweze kupata taarifa zaidi kuhusu mkaa huu, sambamba na kuainisha changamoto zinazorudisha nyuma kasi ya uzalishaji ili kuweza kutatua changamoto hizo kwa pamoja .

Naye Naibu Waziri wa Madini Dkt.Kiruswa ameishukuru Kamati kwa kutembelea mradi huo muhimu na kushukuru kwa ushauri na maelekezo yaliyotolewa yakilenga kuujenga mradi huo ili uwe imara zaidi.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse alipata fursa ya kutoa taarifa ya mradi pamoja na faida zake zikiwemo kuongeza mapato ya Shirika, kuokoa misitu, kuchangia kodi, kutoa ajira na kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Aidha, amekiri kuyatekeleza maoni na maelekezo yote yaliyotolewa na Waheshiwa Wabunge.

Viongozi wengine walioshiriki kwenye ziara hii ni pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Madini na STAMICO, Mameneja na wataalamu kutoka STAMICO ambao ndio wasimamizi mradi huo.