Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

Maendeleo katika Uchorongaji


Wizara ya Madini kwa kushirikiana na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa pamoja wamezindua kiwanda kipya cha mfano cha uchenjuaji wa Madini aina ya dhahabu kilichopo katika eneo la ITUMBI, Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.

Kiwanda hiki ni muendelezo wa Shirika hilo kuwafikia wachimbaji wadogo wa madini kwa lengo la kuwapatia mafunzo ili waweze kuchimba kitaalamu zaidi Kama Serikali inavyoelekeza.

Mafunzo yatakayotolewa kwenye kiwanda hiki ni pamoja na utafutaji, uchimbaji, uchenjuaji ikiwa pamoja na kuhusisha biashara ya madini.

Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo akiwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo ametoa wito kwa wachimbaji wadogo wa Itumbi na maeneo jirani kukitumia kiwanda hicho kwa ajili ya kujifunza na kupata taarifa mbalimbali zinazohusiana na shughuli za utafutaji, uchimbaji, uchenjuaji pamoja na biashara ya madini kwasababu Serikali imejemga kiwanda hicho kwa ajili ya kuboresha shughuli zao za uchimbaji Madini
Tanzania Census 2022