Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

MATOKEO CHANYA YA STAMICO YAIFANYA KUWA TOFAUTI NA ZAMANI


Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko aeleza jinsi Shirika la Madini la Taifa ( STAMICO) lilivyochangia katika mafanikio ya Sekta ya Madini.

Ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari Kuhusu Mafanikio ya Mwaka Mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita Madarakani,Jijini Dodoma.

Amesema kupitia Maonesho Makubwa ya Biashara ya Dubai Expo2020 Serikali kupitia STAMICO imesaini mkataba wa uchorongaji kati yake na Buhemba Gold Company wenye thamani ya shilingi bilioni 11.5. ili kuchoronga mita 10,000 za miamba kwa teknolojia ya DD na mita 30,000 kwa teknolojia ya RC. Mkataba mwingine ni wa makubaliano ya utafiti na uendelezaji wa leseni za madini za Shirika na kampuni ya ACME ya Singapore wenye thamani ya karibu Dola za Marekeni milioni 300.

Tayari Shirika limefanya uchorongaji katika mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML) wenye thamani ya shilingi bilioni 18 na katika Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) shilingi bilioni 1.4. Aidha, STAMICO imefanya ukarabati wa mgodi wake wa chini wa makaa ya mawe Kiwira ili uweze kuendelea na uzalishaji wa makaa hayo.

Biteko amebainisha kuwa, STAMICO imefanikiwa kuanza uzalishaji mkubwa wa dhahabu katika Mgodi wa dhahabu wa Buckreef uliopo Geita; kuendeleza mradi wa kuchimba Dhahabu Buhemba kwa kutengeneza miundombinu ya mgodi, kuagiza mtambo na shughuli za uchorongaji.

Shirika limeweza kutoa gawio Serikalini la jumla ya Shilingi bilioni 1.2 katika mwaka wa fedha 2020/21.

Amesema, STAMICO imeendelea kuwa mlezi wa wachimbaji wadogo ili hatimaye waweze kukua na kuongeza tija katika kufanya shughuli zao.

Aliendelea kusema, STAMICO imesaini mikataba na benki mbalimbali za biashara nchini kwa ajili ya kuwasaidia wachimbaji wadogo kupatiwa mikopo na kuwaunganisha na benki kadhaa, zikiwemo Benki za NMB, KCB na CRDB, hivyo wadau wote mnahamasishwa kuzichangamkia fursa

"Kwa hakika, ipo tofauti kubwa sana kati ya STAMICO ya sasa na ya zamani kutokana na matokeo makubwa ambayo shirika hili linaendelea kufanya. Kupitia juhudi hizi, Shirika lilifanikiwa kukusanya shilingi bilioni 19.97 kati ya Machi 2021 na Februari 2022 kutoka vyanzo vyake vya ndani.