Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

MKURUGENZI MTENDAJI WA STAMICO ASHIRIKI KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UWEKEZAJI LINALOFANYIKA ZANZIBAR


Mkurugezi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse leo tarehe 7 Disemba 2021 pamoja na viongozi wengine kutoka Wizara ya Madini na Sekta binafsi kwa pamoja wamehudhuria kongamano hilo lililofanyika katika hoteli ya Golden Tulip,Zanzibar.

Kongamano hilo limefunguliwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi.

Katika hotuba yake ya ufunguzi Rais Mwinyi amesema kwa sasa Serikali imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwa pande zote mbili bara na visiwani hivyo kuwaalika wawekezaji kujitokeza kwa wingi kuwekeza kwenye sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Madini, Utalii, Miundombinu na kadhalika.

Amesema Tanzania ina sera na sheria bora kwa ajili ya kuwavutia wawekezaji hivyo kuwataka wasisite kuwekeza Tanzania.

Viongozi wakuu ambao wawameshiriki Kongamano hilo kutoka Wizara ya Madini ni pamoja na Kamishna wa Madini, Dkt Abdulhaman Mwanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Dkt. Mussa Budeba, na makamu wa rais kutoka GGM Bw. Simon Shayo.

Kongamano hili linaenda sambamba na maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara na Maonesho ya Bidhaa za Viwandani yanayofanyika katika viwanja Maisara.

Kongamano hili limewakutanisha wawekezaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ya Tanzania ambapo Shirika la Madini la Taifa ni moja ya wafadhili wa kongamano hili.