Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

MTAMBO MPYA WA KISASA WA STAMICO WAWA KIVUTIO KATIKA MKUTANO WA JUKWAA LA USHIRIKISHWAJI WATANZANIA SEKTA YA MADINI



Leo tarehe 20 Mei 2022 Shirika la Madini la Taifa (Stamico) limeshiriki jukwaa la kwanza la ushirikishwaji Watanzania katika Sekta ya Madini linalofanyika Jiji Mwanza kuanzia tarehe 20 - 22 Mei 2022. Aidha jukwaa hilo lilienda sambamba na Maonesho ya Madini.


Mgeni rasmi wa jukwaa hilo alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini Profesa Kikula kwa niaba ya Waziri wa Madini Mhe Dkt Doto Biteko. Aidha kupitia jukwaa hilo wageni mbalimbali waliweza kutembelea banda la STAMICO kujionea bidhaa na shughuli za Shirika.


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dr. Venance Mwasse wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi alisema Shirika limepata mafanikio makubwa katika dhana ya ushirikishwaji Watanzania alisema Shirika limekuja na bidhaa yake mpya sokoni Mkaa mbadala wa Rafiki briquettes ambao utasaidia sana kudhibiti ukataji miti . Alimweleza Mgeni rasmi kwamba mtambo wa majaribio umeshasimikwa na uzalishaji wa majaribio umeshaanza na kupata cheti cha ubora kutoka TBS kimeshapatika.


Aidha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO alimueleza Mgeni rasmi juu ya biashara ya uuzaji wa kemikali na vilipuzi ikiwalenga wachimbaji wadogo na wakubwa.


Nae Mgeni rasmi Profesa Kikula amesifia STAMICO jinsi linavyoshiriki katika kuinua sekta ya Madini na kuchangia pato la Taifa.
Jukwaa hili litafungwa rasmi tarehe 22 Mei 2022