Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

​STAMICO, BUCKREEF ZA SAINI MKATABA MNONO WA UCHORONGAJI.


Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) leo tarehe 30 Agosti 2021 limesainiana mkataba wa kandarasi ya uchorogaji miamba na Kampuni ya Madini ya Buckreef Gold Company Ltd inayochimba madini ya Dhahabu mkoani Geita yenye thamani ya Billion 4.

Makubaliano hayo yamefanyika leo katika ofisi za STAMICO, zilizopo jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Madini na STAMICO.

Aidha Mgeni rasmi kwenye tukio hili alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila.

Katika hotuba yake Katibu Mkuu ameipongeza STAMICO kwa kazi nzuri wanayofanya ya uchorongaji ambayo imewafanya kupata tena kandarasi hii kubwa ya uchorongaji. "Kandarasi hii ni kubwa kwa hiyo fanyeni kazi hii kwa viwango vya juu kwa kutumia ujuzi wenu wote, kwa uaminifu na bidii" amesema Katibu Mkuu.

Naye Kaimu Mkurugezi Mtendaji wa STAMICO, Dr Venance Mwasse ameishukuru Wizara ya Madini kwa kuendelea kuiamini STAMICO na kumhakikishia Katibu Mkuu, kufanya kazi hii ya uchorongaji kwa weledi na kwa kufuata vigezo vyote vilivyopo kwenye mkataba.

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Buckreef, Bw.Khalaf Rashid ameishukuru Wizara ya Madini na STAMICO kwa kuendelea kufanya kazi kwa karibu na kampuni ya Buckreef.

Utiaji saini umefanyika baina ya STAMICO na Kampuni ya Dhahabu Buckreef na kushuhudiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Madini, viongozi kutoka Wizara ya Madini, STAMICO na Tume ya Madini.