Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO WATOA ELIMU KWA WAJASIRIAMALI NA WACHIMBAJI MADINI WANAWAKE LINDI


Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa semina ya matumizi ya nishati safi na salama afisa masoko wa STAMICO Bw. Mark stephano amewataka wanawake kutumia mkaa wa nishati mbadala unaotokana na makaa ya mawe (Rafiki Briquettes) ili kulinda afya zao na kulinda mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Kwa upande wa mwenyekiti wa wachimbaji madini wanawake Tanzania Bi Palina Ninje amewataka wanawake hao kutumia fursa ya kibiashara kwa kuuza mkaa mbadala wa Rafiki Briquettes vijijini ili kuzidi kujikwamua kiuchumi. Mafunzo haya ya siku mbili (2) yalikuwa na lengo la kuelimisha wanawake wajasiriamali mkoani Lindi kunufaika na mnyororo wa Biashara ya nishati safi na salama ya Rafiki Briquettes inayozalishwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).