Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO YAINGIA MAKUBALIANO MENGINE NA BENKI YA CRDB


Ikiwa ni mwanzoni kabisa mwa mwaka 2022, Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko ameshuhudia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) pamoja na Benki ya CRDB wakitiliana saini Makubaliano ya Awali ya Kuwasaidia Wachimbaji Wadogo Kupata Mikopo.

Tukio hilo limefanyika wakati wa Mkutano Mkuu wa 24 wa Chama cha Wachimbaji Wanawake Tanzania (TAWOMA) uliofanyika jijini Dodoma.

Akizungumza wakati akifungua Mkutano huo, Waziri wa Madini Dkt. Biteko amezipongeza taasisi hizo STAMICO na Benki ya CRDB zikiwemo taasisi nyingine za fedha kwa kubadilisha mtazamo dhidi ya wachimbaji wadogo na kuamua kuwakopesha.

Amesema STAMICO ina jukumu kubwa la kuthibitisha taarifa za jiolojia za wachimbaji wadogo kwa kuwa daraja kwa wachimbaji wadogo katika kupata mikopo kutoka katika taasisi za fedha.

Ametumia nafasi hiyo kuwapongeza wanachama wa TAWOMA na kuwataka kuwa vinara katika sekta ya madini ili kuondoa dhana ya unyonge wanapokuwa katika kazi zao katika mnyororo wa uchimbaji madini.

Amesema wanawake ni hazina kubwa kwa Taifa kwa kuwa wana uwezo wa kufanya kazi zaidi ya moja kwa wakati mmoja, wana kiwango kikubwa cha uaminifu na kwamba wanawake wakishirikishwa vizuri katika mnyororo wa uchimbaji madini itainufaisha jamii nzima ya Watanzania.

Amewataka wanawake hao kutosahau jukumu lao la malezi kwa familia zao wakati wanatekeleza shughuli za uchimbaji ili kuweza kujenga jamii yenye tabia nzuri na kukubalika katika jamii. Pia, amewataka

kukemea tabia ya kulalamika na badala yake kuwajenga katika kujituma na kujisimamia.

Akzungumza kama Mlezi wa Wachimbaji Wadogo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse ameishukuru Benki ya CRDB kwa kukubali kuwasaidia Wachimbaji Wadogo kupata mikopo ambayo imekuwa kilio kikubwa cha muda mrefu kwa Wachimbaji Wadogo.

Ametoa pongezi kwa wanawake wachimbaji (TAWOMA) na kuwekeza kuwa wana nguvu ya uthubutu, ubunifu na ujasiri wa kujikita katika sekta hiyo ya uchimbaji mdogo ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikiaminika ni maalum kwa ajili ya wanaume tu.

“Niliwahi kukaa na kina mama wa TAWOMA wakanielezea mikakati yao, kwa kweli kina mama hawa wana maono ya mbali sana