Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO YAPATA BODI MPYA


Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limepata Bodi mpya ya Wakurugenzi itakayodumu kwa muda wa miaka 3 kuanzia 2021-2024.

Bodi hiyo mpya inaongozwa na Mwenyekiti Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo ambaye ameteuliwa tena na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mapema Disemba 2021 ikiwa na wajumbe nane ambao ni Bw.Saidi A. Nzori, Bi. Janeth Luponelo, Bw. Emmanuel M. Shubi. Bi. Prisca Lwangili, Bw. Lukas Selelii, Bw. Abdul-Razaq Badru, Bw. Leonard Kitoka na Bi. Yokbeth F. Myumbilwa.

Wajumbe wa Bodi hiyo wameteuliwa na Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko kwa mujibu wa kifungu Na.6 (1) cha hati ya uanzishwaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) cha mwaka 1972 kinachompa mamlaka Waziri wa Madini kuteua wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi.

Akiongea mara baada ya uteuzi huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse amesema amefurahishwa na uteuzi huo kwa kuwa asilimia kubwa ya wajumbe walioteuliwa kwenye Bodi hiyo walikuwepo kwenye Bodi iliyopita na walikuwa na mchango mkubwa sana wa mageuzi katika kulipa taswira mpya Shirika la Madini la Taifa.

“Nina matumaini makubwa na Bodi hii mpya kwa kuwa wajumbe wengi walioteuliwa tumefanya kazi nao katika Bodi iliyopita, hivyo tunaenda kuendelea pale tulipoishia." Amesisitiza Dkt. Mwasse

Bodi iliyopita ilifanya kazi kwa weledi na ufanisi mkubwa na tuliweza kushirikiana bila shida yoyote. Iliweza kutoa maelekezo yenye tija na kutekelezeka katika kutatua changamoto mbalimbali za Shirika”

STAMICO inaahidi ushirikiano kwa Bodi hii mpya ili kuendelea kutekeleza miradi yake kwa ufanisi ili kufikia malengo iliyojiwekea.

STAMICO ina mategemeo makubwa na Bodi katika kutekeleza majukumu yake.