Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO YAPATA MKATABA MNONO WA UCHOROGAJI KUTOKA TGDC

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) laanza kufanya uchorongaji katika mradi wa jotoardhi baada ya kutia saini ya Mkataba unaohusu uchorongaji wa visima vifupi vitatu baina yake na Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) katika hafla ya utiaji saini iliyofanyika leo tarehe machi 1, 2021 jijini Mbeya.

Akiongea kuhusu mkataba huo Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof, Simon Msanjila amesema kwa sasa STAMICO inaweza kufanya uchorongaji wa kila aina kwa kuwa ina mitambo ya kisasa inayoweza kukidhi mahitaji ya wateja wake na kukamilisha kwa muda muafaka.

Awali Prof, Msanjila alielezea historia fupi ya STAMICO ilivyopitia changamoto hadi ilipofikia na kumesema; kwa sasa hana wasiwasi na Shirika hilo katika kutekeleza matakwa ya mkataba huo kwa kuwa lina vifaa vya kutosha na uthubutu katika utendaji kazi wake.

Amefurahishwa kuona taasisi hizi mbili za Serikali zimebadilika kiutendaji na kuanza kufanya kazi za kibiashara pamoja ili kufikia malengo yao, amesema taasisi hizi mbili zinastahili pongezi na kuzitaka zizidi kufanya kazi kwa bidii na uthubutu ziweze kwenda mbali zaidi.

Aidha ametumia nafasi hiyo kuipongeza Bodi ya STAMICO inayooShirika la Madini la Taifa (STAMICO) laanza kufanya uchorongaji katika mradi wa jotoardhi baada ya kutia saini ya Mkataba unaohusu uchorongaji wa visima vifupi vitatu baina yake na Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) katika hafla ya utiaji saini iliyofanyika leo tarehe machi 1, 2021 jijini Mbeya.

Akiongea kuhusu mkataba huo Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof, Simon Msanjila amesema kwa sasa STAMICO inaweza kufanya uchorongaji wa kila aina kwa kuwa ina mitambo ya kisasa inayoweza kukidhi mahitaji ya wateja wake na kukamilisha kwa muda muafaka.

Awali Prof, Msanjila alielezea historia fupi ya STAMICO ilivyopitia changamoto hadi ilipofikia na kumesema; kwa sasa hana wasiwasi na Shirika hilo katika kutekeleza matakwa ya mkataba huo kwa kuwa lina vifaa vya kutosha na uthubutu katika utendaji kazi wake.

Amefurahishwa kuona taasisi hizi mbili za Serikali zimebadilika kiutendaji na kuanza kufanya kazi za kibiashara pamoja ili kufikia malengo yao, amesema taasisi hizi mbili zinastahili pongezi na kuzitaka zizidi kufanya kazi kwa bidii na uthubutu ziweze kwenda mbali zaidi.

Aidha ametumia nafasi hiyo kuipongeza Bodi ya STAMICO inayoongozwa na Meja Jenerali mstaafu Micheal Isamuyo kwa kuwa na maono ya ushindani na mafanikio licha ya changamoto nyingi ambazo Shirika limepitia wakati Bodi hii inaanza kazi ya kulisimamia.

Ameahidi kuendeleza ushirikiano ili kuleta mafanikio katika upande wa uchorongaji kwa kuongeza mitambo mikubwa na kusema kuwa Serikali ipo katika mchakato wa kununua mtambo mkubwa ambao unahitajika ili kufanya kazi kubwa zaidi na kuwafikia wateja wengi ambapo sasa hakutakuwa na sababu ya kutumia kampuni zingine na kuicha STAMICO.

Naye Kaimu Mkurugenzi STAMICO, Dkt. Venance Mwasse ameshukuru kupata kandarasi hii na kusema kuwa ni fursa ya kibiashara ambayo itaisaidia STAMICO kuendelea zaidi kwa kuijengea imani kwa wateja wengine hivyo ameahidi kuikamilisha kazi hii kwa wakati kutokana na uzoefu katika kazi za uchorongaji.

Amesema STAMICO imepokea kwa furaha kazi hii ya kuchoronga visima vitatu vifupi vya utafiti vyenye jumla ya mita mia tisa na kuahidi kuifanya kazi hii kwa uweledi na ufanisi ili kuleta tija kwa kampuni ya TGDC.

Aidha Meneja Mkuu wa Kampuni ya TGDC Mha. Kato Kabaka amesema mkataba huu ni matokeo ya utafiti uliokwishafanyika na kuonesha eneo hilo lina vigezo vya upatikanaji wa joto litalowezesha kuzalisha umeme ikiwa ni moja ya jitihada za kampuni hiyo katika kutafuta njia mbadaka ya kuzalisha umeme kwa kutumia jotoardhi.

Amesema uchorongaji huu unatarajia pia kuwanufaisha wanajamii kutokana na kuwepo kwa fursa za ajira, uboreshaji wa miundo mbinu ili kutengeneza mazingira wezeshi ya mradi huo. Ameahidi kutoa ushirikano kwa mkandarasi ambaye ni STAMICO ili kusaidia kandarasi hii kukamilika.

STAMICO imeendelea kujitanua kibiashara kwa kuanza kuanza uchorongaji wa utafiti wa joto ardhi licha ya kubobea katika uchongaji wa utafiti wa madini mafuta na gesi.

Mapema mwezi Machi 2021, STAMICO imesaini mkataba wa uchorongaji katika hafla fupi iliyohudhuriwa na viongozi wakuu wa wizara wakiwemo Makatibu Wakuu Wizara ya Madini na Wizara ya Nishati, Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO, Watendaji wakuu, watendaji na wataalamu kutoka STAMICO na TGDC na pia wanahabari. Mkataba huo una thamani ya shilingi bilioni 1.1 unahusiana na uchorongaji wa Visima Vitatu vya Utafiti katika Mradi wa Jotoardhi uliopo Kijiji cha Kiejo-Mbaka wilayani Rungwe mkoa Mbeya. Mkataba huu unataraji kudumu kwa muda siku tisini.ngozwa na Meja Jenerali mstaafu Micheal Isamuyo kwa kuwa na maono ya ushindani na mafanikio licha ya changamoto nyingi ambazo Shirika limepitia wakati Bodi hii inaanza kazi ya kulisimamia.

Ameahidi kuendeleza ushirikiano ili kuleta mafanikio katika upande wa uchorongaji kwa kuongeza mitambo mikubwa na kusema kuwa Serikali ipo katika mchakato wa kununua mtambo mkubwa ambao unahitajika ili kufanya kazi kubwa zaidi na kuwafikia wateja wengi ambapo sasa hakutakuwa na sababu ya kutumia kampuni zingine na kuicha STAMICO.

Naye Kaimu Mkurugenzi STAMICO, Dkt. Venance Mwasse ameshukuru kupata kandarasi hii na kusema kuwa ni fursa ya kibiashara ambayo itaisaidia STAMICO kuendelea zaidi kwa kuijengea imani kwa wateja wengine hivyo ameahidi kuikamilisha kazi hii kwa wakati kutokana na uzoefu katika kazi za uchorongaji.

Amesema STAMICO imepokea kwa furaha kazi hii ya kuchoronga visima vitatu vifupi vya utafiti vyenye jumla ya mita mia tisa na kuahidi kuifanya kazi hii kwa uweledi na ufanisi ili kuleta tija kwa kampuni ya TGDC.

Aidha Meneja Mkuu wa Kampuni ya TGDC Mha. Kato Kabaka amesema mkataba huu ni matokeo ya utafiti uliokwishafanyika na kuonesha eneo hilo lina vigezo vya upatikanaji wa joto litalowezesha kuzalisha umeme ikiwa ni moja ya jitihada za kampuni hiyo katika kutafuta njia mbadaka ya kuzalisha umeme kwa kutumia jotoardhi.

Amesema uchorongaji huu unatarajia pia kuwanufaisha wanajamii kutokana na kuwepo kwa fursa za ajira, uboreshaji wa miundo mbinu ili kutengeneza mazingira wezeshi ya mradi huo. Ameahidi kutoa ushirikano kwa mkandarasi ambaye ni STAMICO ili kusaidia kandarasi hii kukamilika.

STAMICO imeendelea kujitanua kibiashara kwa kuanza kuanza uchorongaji wa utafiti wa joto ardhi licha ya kubobea katika uchongaji wa utafiti wa madini mafuta na gesi.

Mapema mwezi Machi 2021, STAMICO imesaini mkataba wa uchorongaji katika hafla fupi iliyohudhuriwa na viongozi wakuu wa wizara wakiwemo Makatibu Wakuu Wizara ya Madini na Wizara ya Nishati, Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO, Watendaji wakuu, watendaji na wataalamu kutoka STAMICO na TGDC na pia wanahabari. Mkataba huo una thamani ya shilingi bilioni 1.1 unahusiana na uchorongaji wa Visima Vitatu vya Utafiti katika Mradi wa Jotoardhi uliopo Kijiji cha Kiejo-Mbaka wilayani Rungwe mkoa Mbeya. Mkataba huu unataraji kudumu kwa muda siku tisini.