Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

MJI WA YANGKANG JIMBO LA JINHUA NCHINI CHINA WAVUTIWA KUJA KUWEKEZA KWENYE SEKTA YA MADINI TANZANIA


Mnamo tarehe *15 Agosti, 2023* Ujumbe wa Wizara ya Madini ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Bw. Msafiri Mbibo umekuwa na mazungumzo na Uongozi wa Biashara na Uwekezaji wa Mji wa Yongkang (Yongkang Bureau of Commerce) chini ya Bi. Zhang You you ambaye ni Mwenyekiti wake.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika kituo cha uwekezaji Leo la Kikao hicho ilikuwa kutengeneza mazingira wezeshi na kujenga mashirikiano ya kibiashara na uwekezaji kwenye Madini na nyanja nyingine za kiuchumi.

Akizungumza kwenye Kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse amewakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji wa mji wa Yongkang kuja kuwekeza nchini Tanzania hususani kwenye uchimbaji na uongezaji thamani madini hususani madini ya Kimkakati na Madini ya Viwandani kwani kupitia Serikali ya Awamu ya Sita mazingira ya kibiashara na uwekezaji yameboreshwa zaidi.

Mbali na hilo, Tanzania ni nchi iliyojaliwa kuwa na aina nyingi za madini yakiwemo madini ya kimkakati na madini ya viwandani ambayo ni malighafi ya viwandani.

Kwa kuwa mji wa Yongkang una viwanda vingi vinavyotegemea malighafi ambayo kwa sehemu kubwa ni Madini mfano madini ya aluminum,copper, manganise, tin, colbalt, lithium na mengine mengi ambayo yanapatikana kwa wingi Tanzania.

Aidha, Dkt. Mwasse amewahidi wafanyabiashara na wawekezaji kutoka mji huo ya kuwa Shirika litatoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha malengo haya.

Aidha, Kwa upande wa vifaa na teknolojia kwenye Uchimbaji wa Madini STAMICO ipo tayari kuwezesha wawekezaji hawa kupata wateja ambao ni Wachimbaji Wadogo wa Madini chini ya Ulezi wa Shirika.

Hivyo, Dkt. Mwasse aliwaomba wawekezaji na wafanyabiashara kutoka mji huo kufungua ofisi na magara (wherehouse) Tanzania itakayorahisisha hupatikanaji wa huduma na vifaa kwa Wachimbaji Wadogo na STAMICO ipo tayari kuwawezesha (facilitate) kufanya hivyo katika kila hatua.

Akiongea Kwa upande wa Chemba ya Biashara na Uwekezaji wa Mji Yongkang Ms. Zhang ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Chemba hiyo aliishukuru Serikali ya Tanzania kupita Wizara ya Madini Kutembelea Mji huu na kutaka kuwepo na mashirikiano ya kibiashara.

Uongozi wa mji pamoja na sekta binafsi upo tayari kutoa kila aina ya ushirikiano hususani kwenye biashara ya Madini upande wa teknolojia, vifaa na zana za Uchimbaji na uongezaji thamani Madini.

Bi. You you al aliahidi kwa kushirikiana na sekta binafsi ya mji wake watahakikisha wanafungua ofisi mwishoni mwa mwaka huu 2023 na kabla ya hapo watatuma wawakilishi wao mwezi september kuja nchini Tanzania kwa ajili ya maandalizi na kuangalia fursa zaidi za uwekezaji na biashara.

Katika siku za Hivi karibuni wataingia makubaliano ya awali (MoU) na STAMICO ili kuwa na mashirikiano kwenye Uchimbaji na biashara ya Madini.

Kikao hiki kimehudhuriwa na Watendaji wa Wizara ya Madini na Taasisi zake, FEMATA na Benki ya CRDB, Touchroad, Viongozi wa Serikali na Sekta binafsi ya mji wa Yongkang.

Kikao hiki kinafanyika ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya Wachimbaji na Wadau wa Madini kutoka Tanzania zaidi ya 100 nchini China iliyoanza tarehe 12 Agosti 2023 inayotarajiwa kukamilika tarehe 24 Agosti, 2023.