Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

Ushindi wa kishindo Geita


Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeibuka na Tuzo Tatu baada ya kushinda katika makundi matatu tofauti wakati wa maonesho ya Nne ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yaliyoanza 16- 26 Septemba 2021, Mkoani Geita.


Tuzo hizo zimetolewa septemba 26, 2021 na Waziri wa Fedha Dkt.Mwigulu Nchemba kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Isdor Mpango wakati akihitimisha maonesho hayo ambapo STAMICO imejitwalia ubingwa namba moja kwa Makampuni ya Uchimbaji Madini, na kuchukua Tuzo ya Mshindi wa Pili kwa Banda Bora na Taasisi Wezeshi katika Sekta ya Madini.

Pamoja na tuzo hizo STAMICO imepokea Hati ya Pongezi na Shukrani kwa kudhamini maonesho ya Madini 2021.


Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Bw. Geofrey Meena amesema amejawa na furaha sana kupokea tuzo hizo tatu ambazo zimekuwa ni chachu katika utendaji kazi hususani katika kuwaendeleza wachimbaji wadogo, ubunifu wa bidhaa na miradi mipya
Amesema ushindi huu umechochewa na mambo mbalimbali ikiwemo kuleta vitu vinavyosadifu kauli mbiu ya maonesho ya mwaka huu kwa kujikita katika Kiwanda cha kusafisha Dhahabu kilichopo mwanza, uzalishaji wa Mkaa Mbadala wa makaa ya mawe na vituo vya mfano kwa wachimbaji wadogo ambavyo vimeshatoa matokeo chanya.

Ameongeza kuwa Shirika limetumia ubunifu mkubwa katika kuwasilisha elimu kwa wadau mbalimbali waliotembelea banda na kutengeneza mpangilio mzuri wa banda na kufanya livutie.

Licha ya ushindi huo STAMICO imetumia imekuwa ikitumia maonesho hayo kukusanya maoni na ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali ili kuweza kuboresha shughuli za kila siku na kujenga Shirika.


“Tumekuwa tukitumia Maonesho haya kutoa elimu kwa wananchi lakini pia kukusanya maoni na mapendekezo kutoka kwa wadau ili kujenga.” Aliongeza Meena


Ameahidi kuendelea kushiriki katika Maonesho haya kwa kuwa yanatoa hamasa na elimu kwa pande zote mbili.