Rafiki Briquettes ni nini?
Rafiki Briquettes ni nini?
Rafiki Briquettes ni bidhaa ya mkaa inayotokana na makaa ya mawe yanayozalishwa na STAMICO kupitia viwanda vyake vya Kiwira, Kisarawe na Tirdo.Bidhaa hii ni rafiki kwa matumizi ya majumbani, kwenye taasisi mbalimbali na sehemu za biashara ya chakula, kwani ni nafuu kwa bei na unadumu kwa muda mrefu. Pia ni mkaa rafiki kwa mazingira kwasababu hautoi moshi ambao unaathiri afya za watumiaji ukilinganisha na matumizi ya mkaa utokanao na miti.