Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

MKURUGENZI MTENDAJI DKT. MWASSE AHIMIZA UWAJIBIKAJI NA USHIRIKIANO, STAMICO.


  • Aishukuru Serikali ya Jamhuri Muungano wa Tanzania kwa Kumuamini na kuahidi kuongeza ubunifu
  • Aishukuru Wizara ya Madini na wadau katika sekta kwa ushirikiano wanaoutoa
  • Awashukuru Wana STAMICO kwa kuwa nguzo imara katika kuleta mafanikio
  • Ataka kila mmoja kujiweka sawa ili kuendana na kasi ya utendaji kazi

Mkurugezi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse amewahimiza watumishi wa STAMICO kufanya kazi kwa bidii, kujituma na kuzidisha ushirikiano ili kufikia malengo ya Shirika

Ameyasema haya wakati wa hafla fupi ya kumpongeza kwa kuteuliwa na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kuliongoza Shirika hilo iliyoandaliwa na watumishi wa STAMICO.

Dkt Mwasse amesema amepokea uteuzi huo kwa heshima kubwa na kuahidi kuitumikia nafasi hiyo kwa uadilifu, bidii na ubunifu mkubwa ili kulifanya Shirika lizidi kung'ara, kuaminika zaidi kuleta tija.

Amesema nafasi hiyo ina maana kubwa sana na imekuwa chachu katika utendaji kazi wake na kamwe hatarudi nyuma katika kuhakikisha rasilimali madini zinawanufaisha watanzania kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na STAMICO.

Ameongeza kuwa, hatua hii ni mwanzo wa safari ya ushindi kwa Shirikia na kila mtumishi kwa kuwa sasa Shirikia limeongezewa nguvu akilinganisha na gari lililoongezewa mafuta full tank baada ya kuishiwa mafuta.

Ametoa wito kwa watumishi kufanya kazi kwa bidii bila kuchoka, kuongeza ubunifu na uwajibikaji ili kuhakikisha shirika linapata matokeo chanya.

Aidha amewashukuru wana STAMICO kwa kumuamini na ushirikiano waliompa tangu alipoanza kukaimu nafasi hiyo mwaka 2019 hadi hivi sasa na kuongeza kuwa haya ni mafanikio ya wote.

Amesema watumishi ndio wamemuwezesha kufikia mafanikio hayo kwa kuwa wamekuwa wakifanya kazi bidii , weledi, na ubunifu.

Naye Deusdedith Magala Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala ametoa pongezi na kumuelezea Dkt.Mwasse kuwa ni mtu mwenye udhubutu na ujasiri mkubwa katika utendaji kazi.

Nao watumishi hawakusita kuelezea furaha zao kufuatia uteuzi huo ambapo Mohamed Kaunya ametoa pongezi kwa kuelezea namna Dkt.Mwasse alivyoweza kuleta mabadiliko ya kiutendaji na mafanikio ya Shirika ndani ya mda mfupi.

Mjiolojia Denis Silas amempongeza kwa kuwa na maono makubwa kwa Shirika na kumlinganisha Mkurugenzi huyo na kiungo mchezeshaji katika mpira wa miguu na kuongeza kuwa anastahili kupata nafasi hiyo.

Aidha bi. Misky Masawe mhasibu mwandamizi amempongeza Mkurugenzi huyo na kumuaidi ushirikiano katika kuleta mafanikio ya Shirika

Dkt.Mwasse ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji mnamo Agosti 2022 katika nafasi ambayo amekaimu kwa muda usiozidi miaka mitatu.