Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

RAFIKI BRIQUETTES YAMFURAISHA WAZIRI WA MALIASIlLI NA UTALII


Leo tarehe 26 Septemba 2022, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeshiriki katika kilele cha uzinduzi mpango mkakati unaelezea fursa za utalii zilizopo kusini mwa Tanzania.


Uzinduzi huo umeambatana na maonesho yaliyofanyika katika Viwanja vya Halmashauri ya Njombe Mji.


Mgeni Rasmi katika ufunguzi huo alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana.Mhe Waziri alipata fursa ya kutembelea banda la STAMICO na kujionea Shughuli mbalimbali zinazofanywa na Shirika.Aidha afisa Masoko Mwandamizi Bw. Bilton Otto alimwelezea Mhe Waziri kwa sasa Shirika limekuja na bidhaa mpya ya Mkaa mbadala unaotokana na Makaa ya Mawe ujulikanao *Rafiki briquettes* ambao utasaidia kupunguza changamoto za uharibifu wa Mazingira kwa Kukata Miti hovyo.


Aidha Bw. Otto aliendelea kuelezea kuwa STAMICO kama mdau mkubwa wa utunzaji wa mazingira wakati wa Sherehe za kilele cha kutimiza Miaka 50 toka kuanzishwa kwake ili zindua program ya kupanda miti katika maeneo mbalimbi kupitia kampeni yake ijulikanayo “ STAMICO na mazingira at 50” ambapo kwa kuanzia Shirika lilipanda miti ipatayo 540 katika eneo la Ipagala,Jijini Dodoma.


Katika hatua nyingine Waziri Balozi Dkt Pindi Chana ameipongeza STAMICO kwa juhudi zake mbalimbali wanazozifanya katika kukabiliana na changamoto ya uharibifu wa Mazingira kwa kuja na ubunifu wa mkaa huo vilevile ameipongeza kwa Kufikisha Miaka 50 toka kuanzishwa kwake.


Mkutano huo wa siku mbili umefungwa rasmi tarehe 26 Septemba 2022 na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt.Pindi Chana.