STAMICO YAWAPATIA WANAWAKE NA SAMIA MAKONTENA YA KUUZIA NA KUHIFADHIA RAFIKI BRIQUETTES KWA MIKOA MITANO YA TABORA, KIGOMA, RUKWA, KATAVI NA SINGIDA
STAMICO YAWAPATIA WANAWAKE NA SAMIA MAKONTENA YA KUUZIA NA KUHIFADHIA RAFIKI BRIQUETTES KWA MIKOA MITANO YA TABORA, KIGOMA, RUKWA, KATAVI NA SINGIDA
21 February, 2026
08:00:00 - 13:00:00
KILOLENI, TABORA
barua@stamico.co.tz
Shirika la Madini la Taifa ( STAMICO ) limewapatia vikundi vya Wanawake na Samia wa Mikoa ya Tabora, Kigoma, Katavi, Rukwa na Singida, makontena kwa ajili ya kuhifadhia na kuuzia Nishati safi ya Rafiki Briquettes.
STAMICO ni mlezi wa vikundi hivyo, hivyo inahakikisha Nishati hii ya kupikia ya Rafiki Briquettes inawafikia Watanzania wengi kwa kupitia usambazaji unaofanywa na vikundi vya Wanawake na Samia.
Utoaji huo wa makontena umefanyika katika eneo la Kiloleni Mkoani Tabora, wakati wa uzinduzi wa Kiwanda cha kuzalisha Nishati hiyo ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Waziri wa Madini, Mhe: Anthony Mavunde.