News
KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA STAMICO KWA UWEKEZAJI WA NISHATI YA KUPIKIA YA RAFIKI BRIQUETTES
Kamati ya NISHATI na MADINI wakiongozwa na Mwenyekiti Mh. Dkt.David Mathayo (MB) leo tarehe 13 Machi walifanya ziara kwenye mradi wa kutengeneza nishati mbadala ya Rafiki Briquettes.
Katika ziara hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse aliwaongoza wajumbe wa kamati kushuhudia shughuli mbalimbali zinazofanyika katika uzalishaji nishati ya Rafiki Briquettes zikiwemo
Uchomaji wa nyama , mahindi ya kuchoma na upikaji wa maharage.
Wajumbe wa Kamati walipongeza mageuzi na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Shirika katika mgodi wa Kiwira na Rafiki Briquettes kwa ujumla.
Wajumbe pia waliridhishwa na maendeleo ya mradi wa nishati safi ya kupikia ya Rafiki Briquette na kusisitiza nishati hiyo muhimu iweze kuwafikia wananchi wengi ili kuendelee kuunga mkono ajenda ya upatikanaji wa nishati safi na nafuu kwa Watanzania wote.
Aidha Mheshimiwa Naibu Waziri wa Madini, Dkt Steven Kiruswa ambae aliambatana na Kamati katika ziara hiyo aliishukuru kamati kwa maoni yao na miongozo mbalimbali wanayoitoa kwa Shirika ambayo imeleta mafanikio makubwa katika mradi wa Rafiki Briquettes kuanzia utafiti wake hadi kwenye uzalishaji.