Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

Hatimaye Mtambo Mpya wa kisasa wa kutengeneza Mkaa Mbadala Umewasili


Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeingiza nchini Mtambo wa kisasa wa kutengeneza Mkaa Mbadala (Rafiki Briquettes)

unaotokana na makaa ya mawe ili kuwa mbadala wa kuni na mkaa utokanao na miti.

Mtambo huo umewasili nchini mwezi Januari, 2022 ukitokea nchini China.

Kwa sasa Mtambo huo umesimikwa kwenye eneo la Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) Msasani, jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuanza uzalishaji.

Mtambo huo ni wa kisasa na una uwezo wa kuzalisha tani mbili za Mkaa mbadala kwa saa kwa ubora wa kiwango cha kimataifa.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse aliweza kutembelea na kukagua zoezi la usimikaji wa Mtambo huo na zoezi hilo limeshakamilika vizuri na uzalishaji wa majaribio (pilot production) utaanza wiki ijayo ya tarehe 17 Januari 2022.

Akiongea baada ta kukagua zoezi la usimikaji Mtambo huo, Dkt. Venance Mwasse alisema "Tunajivunia kupata Mtambo huu mpya na wa kisasa wa kutengeneza Mkaa Mbadala, Mtambo huu tumeungojea kwa muda mrefu, tunashukuru umefika salama na ile ndoto yetu ya kuanza kutengeneza Mkaa Mbadala unatokana na Makaa ya mawe hapa Tanzania imetimia".

Mkaa huu utakuwa suluhisho kubwa kwenye mazingira hususani athari zinazotokana na ukataji miti hovyo kwa ajili ya kupata nishati ya kupikia, hautakuwa na moshi na pia gharama itakuwa rafiki kwa watumiaji ukilinganisha na nishati zingine.

Ubunifu Makini kwa Maendeleo ya Viwanda na Hifadhi ya Mazingira.