Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO yaibuka Mshindi bora Nishati na Madini Sabasaba


STAMICO YAPIGA USHINDI DABO DABO NDANI YA MAONESHO YA 77 , 2021

Shirika la Madini la Taifa ( STAMICO) lapata tena kombe la ushindi katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa almaarufu kama Saba saba Leo Julai 13, 2021 siku ya kufunga Maonesho hayo.

Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Bw. Deusdedith Magala amesema amejawa na furaha furaha mara baada ya kupokea kombe la Pili la MSHINDI Bora katika kipengele cha Nishati na Madini.

Amesema ushindi wa mwaka huu umekuwa ni chachu! katika utendaji kazi wa Shirika amesema ushindi unahitaji Ubunifu mkubwa na kujituma Sana.

Amesema STAMICO ilijizatiti kutoka na ushindi ambapo iliangalia ni vitu lengwa katika kauli mbiu ya Maonesho ambapo mwaka huu ilijikita katika Viwanda vikubwa viwivili Kiwanda cha kusafisha Dhahabu jilichopo mwanza na uzalishaji wa Mkaa Mbadala wa makaa ya mawe.

Ameongeza kuwa Ubunifu mkubwa uliotumika katika uwasilishaji wa taaluma umewafanya watu wengi kujongea katika banda la STAMICO na kupata elimu.

Ameahidi kuyafanyia kazi maoni yote yaliyotolewa na wananchi ili kuweza kujenga Shirika.

Tumekuwa tukitumia Maonesho haya kutoa elimu kwa wananchi lakini pia kukusanya maoni na mapendekezo kutoka kwa wadau ili kujenga.

Ameahidi kuendelea kushiriki katika Maonesho haya kwa kuwa yanatoa hamasa na elimu kwa pande zote mbili