Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

STAMICO YASHIRIKI VIZURI JKT MARATHON 2023


Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeshiriki mbio za marathon (JKT Marathon 2023) ambazo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa-JKT.

Katika kushiriki huko Shirika limepewa medali ya dhahabu ikiwa ni kutambua mchango wake katika kufanikisha maadhimisho ya miaka 60 ya JKT tangu kuanzishwa kwake

Aidha Shirika lilipewa heshima ya kutunuku tuzo mbalimbali kwa washindi wa mashindano ya marathon ya Km 21.

Mgeni rasmi wa mashindano hayo alikuwa Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu kulikwepo na viongozi wengine ikiwa pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Innocent Bashungwa.

Katika hotuba yake Mhe. Waziri ameishukuru STAMICO kwa kufanikisha maadhimisho hayo.

Mgeni rasmi ameliomba Shirika kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kusaidia shughuli za ujenzi wa taifa hususani zile zinazo husu vijana.

Naye Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Akson ameupongeza uongozi wa STAMICO kwa kufanikisha tukio hili kubwa la kihistoria kwa nchi yetu.