Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

WAZIRI MAVUNDE ATEMBELEA KIWANDA CHA MWANZA PRECIOUS METALS REFINERY


Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde (Mb) akiambatana na Kamishna wa Madini Dkt. Abdulrahman Mwanga, pamoja na uwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, ametembelea kiwanda cha Mwanza Precious Metals Refinery cha jijini Mwanza.

Waziri alianza ziara yake kwa kujionea jinsi kiwanda kinavyoendesha shughuli zake katika Idara tofauti tofauti za usafishaji dhahabu.

Baada ya ziara fupi kujionea kiwanda, Mhe. Mavunde alipata fursa ya kukaa na Menejimenti ya Kiwanda na kupata taarifa fupi.

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), liliwakilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Pamoja ya Uendeshaji wa Kiwanda Bw. Deusdedith Magala ambaye alitaarifu Kiwanda kina uwezo wa kununua kiasi chochote cha dhahabu na kinafanya malipo kwa Dola za Marekani.

Mhe. Mavunde aliridhishwa na kazi inayoendelea hapo na alitoa pongezi kwa STAMICO pamoja na Kiwanda na kuahidi kuunga mkono kazi inayoendelea.

Mhe. Anthoy Mavunde, alitoa rai kwa wadau wa madini ya dhahabu kutumia fursa ya kipekee iliyotolewa na Serikali kama kivutio, kwa kupunguza mrabaha kutoka 6% mpaka 4%, na kuondelewa kwa ada ya ukaguzi 1% (Inspection fee) kwa dhahabu itakayo uzwa katika kiwanda cha kusafisha dhahabu.

Pia Mhe. Anthoy Mavunde ametoa rai kwa Kiwanda cha Mwanza Precious Metals Refinery kuongeza jitihada za kupata ithibati ya LBMA.