Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

State Mining Corporation

State Mining Corporation

News

RAFIKI BRIQUETTES YAWAVUTIA WAGENI WA KIMATAIFA


Mkaa mabadala wa Rafiki Briquette unaotengenezwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) umekuwa kivutio kwa wageni mbalimbali waliotembelea banda la STAMICO wakati wa Mkutano wa nne wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini unaofanyika katika kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere.

Hayo yamejidhihirisha wakati Waziri wa Nishati na Madini wa Burundi Mhe.Dkt. Ibrahimu Uwizeye alipotembelea banda la STAMICO na kupata maelezo kuhusu mkaa mbadala unaotokana na madini ya makaa ya mawe.

Mhe.Dkt Uwizeye amesema mkaa huu ni tunu muhimu ambayo itasaidia katika kupunguza ukataji wa miti nchini na kuchangia katika zoezi nzima la utunzaji wa mazingira.

“Burundi imeanza kutengeneza mkaa wa aina hii lakini ni kwa kiwango kidogo ni vizuri tukaanza kushirikiana ili kuweza kupata malighafi za kutengenezea mkaa huu nchini alisema Dkt.Uwizeye

Akitoa mfano wa Burundi Dkt. Uwizeye amesema nchi yake wamenza kuzalisha mkaa wa aina hii ambao hutumia udongo na taka zingine na kuishauri STAMICO kuharakisha katika uzalishaji wake ili uweze kuingia sokoni kwa manufaa ya wananchi.

Kwa upande wa STAMICO Meneja wa Masoko na Uhusiano Bw. Geofrey Meena amesema STAMICO itaendelea kutumia fursa mbalimbali ili kuweza kutoa elimu kuhusu miradi na bidhaa za Shirika kama Mkaa huu mbadala.

Aidha Meneja wa Maendeleo ya Biashara kutoka Zambia Bw. Emmanuel Chipungu amesema mkaa ni hatua nzuri ambayo Tanzania imefikia katika kutunza mazingira

Nao wadau mbalimbali walotembelea banda la STAMICO walikuwa na maoni kuhusu mkaa huu ili uweze kuleta tija kwa wananchi

Tukianza na ndugu Baraka ambaye alionesha kufurahisha na mkaa huo na kuipongeza STAMICO kwa hatua ya kuutengeneza mkaa huu kwa viwango vya juu, amesema ni vizuri jitihada za kuhimiza matumizi ya mkaa zikashirikisha na Wizara ya Nishati ili kuhakikisha unafika hadi vijijini ambako nishati zitokanazo na miti hutumika kwa wingi.

Amesema Serikali iangalie namna bora ya kuhakikisha mkaa huu unawafikia watu wengi kwa gharama nafuu ili kuweza kuleta tija kwa wananchi ambao wanategemea nishati itokanayo na kuni kwa ajili ya kupikia.