Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Shirika la Madini la Taifa

BENKI KUU YA TANZANIA (BOT) YAKOSHWA NA KIWANDA CHA MWANZA PRECIOUS METALS REFINERY

Imewekwa: 17 December, 2025
BENKI KUU YA TANZANIA (BOT) YAKOSHWA NA KIWANDA CHA MWANZA PRECIOUS METALS REFINERY

*Bodi ya Wakurugenzi ya BOT*, ikiongozwa na Gavana ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw. Emmanuel M. Tutuba imetembelea kiwanda cha MPMR, lengo kuongeza uelewa katika shughuli za kiwanda na kujionea mafanikio pamoja na maendeleo ya kiwanda kiujumla.

 

Kwa upande wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), liliwakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance B. Mwasse pamoja na Bw. Deusdedith Magala DHRA-STAMICO na Katibu wa kiwanda cha MPMR.

 

Katika ziara hiyo, Dkt. Venance B. Mwasse alieleza chimbuko la mradi wa MPMR pamoja na manufaa yaliyopatikana ambayo ni pamoja na kuiwezesha BOT kufikia malengo yake ya kununua dhahabu. 

 

Kufuatia kukamilika ziara na wasilisho, Gavana kwa niaba ya Bodi aliridhishwa na kazi inayoendelea kiwandani hapo na alitoa pongezi kwa STAMICO pamoja na uongozi wa MPMR kwa kazi nzuri inayofanyika.

 

Pia Gavana ametoa rai kwa kiwanda cha MPMR kuongeza jitihada za kupata ithibati ya LBMA pamoja na kuongeza mikakati zaidi ya kupata malighafi, ikiwemo kuwawezesha wachimbaji wadogo kifedha.

Awali Bodi ya Bodi ya Ushauri ya Chuo Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ilitembelea kiwanda hicho.

 

Bodi ya Ushauri ya Chuo cha BOT ikiambatana na Makamu Mkuu wa Chuo Dkt. Ephraim Mwasanguti ilitembelea kwa lengo la kujifunza na kujionea jinsi kiwanda kinavyoendesha shughuli zake za uongezaji thamani wa madini ya dhahabu pamoja na fedha kwa viwango vya kimataifa. 

 

Bodi ilifurahishwa na ziara hiyo na kuwa imekuwa na manufaa sana kwa kuwa wameweza kujifunza na kutoa pongezi kwa kiwanda cha MPMR kwa mafunzo na mapokezi waliyoyapata.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo