News
JUKWAA LA NNE LA UTEKELEZAJI WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI LAFUNGULIWA RASMI MWANZA
#STAMICO YAPATA TUZO YA UDHAMINI WA JUKWA HILO
#SERIKALI KUIWEZESHA STAMICO KUSHINDANA NA MAKAMPUNI MAKUBWA YA MADINI DUNIANI
Jukwaa la Nne la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini limezinduliwa rasmi leo Juni 17, 2025 jijini Mwanza ambalo linakutanisha wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Taasisi za Serikali, Taasisi Binafsi, Taasisi za Fedha, Kampuni za Uchimbaji wa Madini na Watoa Huduma kwenye Migodi ya Madini.
Jukwaa hilo lenye kaulimbiu inayosema _*Ongezeko la Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini ni chachu ya Ukuaji wa Uchumi_* linaambatana na maonesho yenye lengo la kuelimisha kuhusu fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini.
Awali kabla ya kufungua Jukwaa hilo Waziri wa Madini Mheshimiwa Antony Mavunde alitembelea Mabanda mbalimbali ya Washiriki wa jukwaa hilo likiwemo Banda la Shirika la Madini la Taifa na kujionea Shughuli mbalimbali zinazofanywa na Shirika na Kuipongeza STAMICO kwa jitihada mbalimbali inazofanya katika uwekezaji kwenye Sekta ya Madini.
Wakati wa hotuba yake ya Ufunguzi wa Jukwaa hilo Waziri Mavunde alisema kwamba Serikali imepanga kuweiwezesha STAMICO nakulifanya Shirika hilo kumiliki migodi yake ya Madini na kushindana na Makampuni Makubwa ya uchimbaji Madini kama Vile GGM na Barick.
Serikali imeipatia leseni ya uchimbaji Mkubwa wa Madini ya Kinywe iliyopo Nachingwea,Mkoani Lindi.
Akiitimisha hotuba ya Ufunguzi Mhe. Waziri aliwakabidhi tuzo Wadhamini wa Jukwaa hilo ambapo tuzo ya STAMICO ilipokelewa na Mkurugenzi Mtendaji Dkt Venance B. Mwasse.
Jukwaa hilo la ushirikishwaji Watanzania katika Sekta ya Madini linatarajiwa kuhitimishwa Tarehe 18 juni 2025.